Dar es Salaam
Wamiliki wa blogu nchini wametakiwa kufuata maaadili ya
uandishi wa habari ikiwemo kuandika habari zenye ukweli na uhakiki ili kuepusha
migogoro isiyo ya lazima kati yao na wananchi.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA), Profesa
John Mkoma alisema hayo jana, alipozungumza na wamiliki wa blogu kuhusu umuhimu
wa kufuata kanuni za kuripoti Uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu
zilizowekwa na mamlaka hiyo.
Profesa Mkoma alisema wanatambua umuhimu wa blogu katika
kuwapa habari wananchi na kuwataka wamiliki hao kupitia kanuni hizo ili
ziwasaidie kujiimarisha kiuandishi.
“Mwaka huu na mwaka ujao ni kipindicha uchaguzi hivyo blogu
hizi zinatakiwa zifuate misingi hiyo katika kuripoti habari hizo za uchaguzi,”
alisema Profesa Mkoma.
Mwandishi wa blogu ya ‘Hivi sasa’, Mgisha Nduguru alisema
kanuni hizo zitawasaidia kujenga uaminifu kwa jamii na kutambulika rasmi kama
chombo cha habari kama yalivyo magazeti na televisheni.
No comments:
Post a Comment