Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Daniel Mkude
(katikati) akisisitiza jambo wakati wa kongamano la Siku ya Nyerere
lililofanyika katika chuo hicho mjini Morogoro jana. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
Mzumbe, Taaluma, Prof. Josephat Itika na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho,
Utawala na Fedha, Prof. Faustin Kamuzora (kulia).
Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watanzania wameshauriwa kuisoma kwa makini Katiba
iliyopendekezwa na lililokuwa Bunge la Katiba ili wasiyumbishwe na kauli
zinazotolewa na watu mbalimbali kwa vile katiba hiyo imetungwa kwa kushirikisha
makundi ya wadau wote hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dkt. Joel Bendera alisema hayo
wakati alipokuwa akifungua Kongamano la siku ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere liloandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe jana mjini Morogoro.
Alisema wananchi waisome vizuri katiba hiyo ili
wasiyumbishwe na kauli zinazoibeza.
“Katiba iliyopendekezwa na bunge la Katiba imetungwa kwa
kufuata misingi ya demokrasia na ilishirikisha wadau wote hapa nchini,”alisema
Alisema katiba hiyo imesheheni maswala yote ya msingi
ukilinganisha na Katika ya mwaka 1977, hivyo ni vyema kuitafakari wakati nchi
ikiwa inaelekea katika kura ya maoni.
Mada kuu ya Kongamano hilo ilikuwa ni ‘Mtazamo wa
Mwalimu kuhusu katiba kama chombo cha kujenga demokgrasia ya kweli.’
No comments:
Post a Comment