Dar es Salaam
Katika juhudi zake za kuendelea
kupendezesha jiji la Dar es Salaam, Benki ya Exim Tanzania imesema inalenga
kupanua zaidi msaada wa kuhudumia bustani mbalimbali.
Benki hiyo, kwa kupitia kampeni yake
ya kupendezesha jiji la Dar es Salaamiliyozinduliwa mwanzoni mwa mwaka 2012,
inatoa mchango mkubwa katika kuhudumia bustani zilizopo katikati ya jiji la Dar
es Salaam.
“Benki inahudumia jumla ya bustani
tatu zilizopo katika maeneo tofauti jijini, ambazo ni pamoja na Bustani ya
Ohio, Clock Tower na Kariakoo.Hadi hivi sasa bustani nyingi zinazohudumiea na
benki yetu zimekuwa zikiwavutia watu wengi na hili limetupa ari zaidi ya
kuzifikia bustani nyingine katika jiji hili,” alisema Afisa Mtendaji wa Benki
hiyo Dinesh Arora.
“Dar es Salaam ni kitovu cha biashara
cha Tanzania ; hii inapelekea uwepo wa wageni wengi wanaotembelea jiji hili.
Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2013,
Tanzania ilipokea zaidi ya watalii milioni moja, ambapo wengi wao walipitia jiji
la Dar es Salaam.
Alisema mchaakto wa kupendezesha
jiji, unaofanywa na Benki ya Exim umelenga kusaidia harakati za serikali na
kuboresha mwonekano wa jiji kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment