Moshi
Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo,
(CHADEMA) ameamua kujenga soko la kisasa
eneo la Kiboriloni litakalo kuwa na vibanda 200 na eneo la wazi kwa ajili ya
wafanyabiashara wa mitumba.
Hata hivyo wakati mbunge huyo akisema hayo,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama alisema mpaka sasa ofisi yake haina
taarifa kama miongoni mwa biashara zitakazorejeshwa ni pamoja na ya mitumba.
Alisema taarifa zilizopo sasa zinasema soko
hilo halitarejeshwa tena katika eneo hilo.
“Awali kulikuwa na soko la mitumba,
likahamishwa na halimashauri tukasema mazingira yale si salama, soko hilo
halipaswi kurejeshwa tena” alisema.
Naye Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar
Michael alisema azimio la Baraza la Madiwani lililotolewa katika kikao cha
Julai, 2011, lilipitisha kuwa soko hilo lirejeshwe. Alisema suala hilo
linakwamishwa na Watendaji wachache kwa maslahi ya kisiasa.
Akizungumza na gazeti hili jana. Ndesamburo
anashangaa kuona serikali ya mkoa ikigoma kurejesha soko hilo la mitumba bila
kutoa sababu za msingi na hata wanazozitoa bado ni nyepesi.
“Nimejenga soko hili ili kuwasaidia
wafanyabiashara wapate eneo la kufanyia biashara. Nataka likikamilika liwe ni
eneo la kisasa la kibiashara ambalo litajulikana ulimwenguni pia” alisema.
No comments:
Post a Comment