Dar es Salaam
Mfanyabiashara maarufu nchini,
Mohammed ‘Mo’ Dewji (39), amezidi kupaa
kwa utajiri, kiasi cha sasa kuwa ndiye bilionea kijana zaidi katika nchi za
Afrika Mashariki, lakini pia akitajwa ndiye bilionea kijana zaidi barani
Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la
Ventures Afrika toleo la juzi, mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mbunge wa
Singida Mjini, anashika nafasi ya 24 ya mabilionea 55 Afrika, wakiongozwa na
Aliko Dangote wa Nigeria.
Dewji anayemiliki kampuni tanzu ya
Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) yenye utitiri wa kampuni, ametajwa
kuwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni 3( Sh trilioni 3.4), hivyo kumfanya
Mtanzania tajiri zaidi, akimpiku Rostam Aziz aliyewahi kutajwa na jarida la
Forbes kuwa ndiye tajiri wa Tanzania.
Kwa sasa, kwa mujibu wa jarida la
Ventures Afrika, Rostam anashika nafasi ya pili kwa utajiri Tanzania akiwa na
utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.2(Sh trilioni 2), lakini kwa Afrika
akishika nafasi ya 40.
Ni Dewji na Aziz tu, ndio Watanzania
pekee katka orodha hiyo ya mabilionea 55 bora Afrika kwa mwaak huu.
No comments:
Post a Comment