Rombo, Kilimanjaro
Shule ya msingi Namfua iliyopo Wilayani hapa Mkoa wa
Kilimanjaro imefungwa kwa kukosa wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Rombo, Elinas Pallangyo aliyasema hayo jana
katika Baraza la Madiwani na kuongeza kuwa, zipo shule nyingine takribani nane ambazo ziko
mbioni kufungwa kwa sababu hiyo.
Pia alisema Halimashauri ya wilaya hiyo amevifunga viwanda 21
vinavyo tengeneza pombe haramu inayodaiwa kupunguza nguvu za kiume.
Alisema viwanda hivyo vilisababisha baadhi ya watu kunywa
pombe hata saa za kazi, alisema kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Wilaya imekuwa
ikipambana na tatizo la pombe haramu, lakini uzalishaji huo ulikuwa unaendelea.
Alisema Rombo imekuwa ikiongoza kwa utemgenezaji pombe haramu
za kienyeji zisizo na viwango.
“Halimashauri imeamua kufunga viwanda 21 vinavyozalisha pombe
hizo zinazo haribu afya za vijana kupunguza uzazi katika Wilaya hii na kukosa
wanafunzi kutokana na uzazi kupungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Pallangyo.
Mkurugenzi wa Halimashauri hiyo, alisema wameziomba Taasisi
za dini kwa jamii hususani madhara ya pombe hizo.
No comments:
Post a Comment