Monday, November 17, 2014

Vodacom yafungua duka Bagamoyo

Pwani
Katika kuhakikisha wakazi wa Bagamoyo mkoani Pwani na maeneo jirani ya Boko na Bunju jijini Dar es slaam wanapata huduma kwa karibu, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imezindua duka jipya katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo.

Bagamoyo ni moja ya miji ya kihistoria nchini yenye vivutio vikubwa vya utalii.

Ulikuwa kituo kikubwa cha biashara ya utumwa ambapo Watalii wengi hupenda kuvitembelea kila mara.

Pia mji huo unatarajiwa kukua kibiashaara kutokana na kuanza kujengwa Bandari kubwa kuliko zote Afrika mashariki na ya kati hivi karibuni.

Duka hilo lenye mazingira rafiki kwa wateja, litatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom,ikiwemo huduma kwa mawakala wa M-Pesa na uuzaji wa bidhaa za kampuni hiyo na litawezesha wateja wa Bagamoyo na wageni watakao tembelea eneo hilo na wateja wa maeneo jirani kama vile Boko na Bunju.
Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya hiyo.


Mkuu wa idara ya mawasiliano na uhusiano wa Vodacom nchini, Rosalynn Mworia, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa wa malengo ya kampuni kuendeleza, kuboresha maisha ya Watanzania na kuwapa huduma bora za kampuni.

No comments: