Dar es Salaam.
Ndoto za wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosoma masomo ya sayansi
ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini ya kuwa magwiji wa fani hiyo
zinaelekea kutimia. Hali hii inatokana na shindano la kusaka vipaji vya
ugunduzi wa program za simu (App Star) mwezi huu.
Shindano hilo la kimataifa lilizinduliwa na Kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania na linajumuisha watanzania wote wenye hamasa ya
kutumia teknolojia kuboresha maisha yao na ya jamii zao kwa ujumla.
Aidha, ngwe ya kwanza ya kuchuja majina ya wale watakao
shiriki katika duru ya mwisho ya mashindano hayo itakayofanyika Bangalore,
nchini India itafanyika Desemba 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania,
Abigail Ambweni aliyekuwa katika harakati za kuwahamasisha wanafunzi wanaosoma
masomo ya komputa katika kitivo cha sayansi ya Komputa cha Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, aliwasihi vijana hao kushiriki katika shindano hilo ambalo pamoja na
mambo mengine pia linalenga kuibua vipaji vya vijana kwenye Nyanja ya ubunifu
wa teknolojia.
No comments:
Post a Comment