Dar es Salaam
Serikali imeipongeza Kampuni ya Vifaa
vya Kielektroniki ya Samsung kwa jinsi inavyoshirikiana nayo kutokomeza
uigizaji wa bidhaa feki nchini.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa
wiki na Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame
Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 4.
Alisema uigizaji wa bidhaa feki una
madhara makubwa na unachangiwa na ubinafsi wa wachache.
“Ni wajibu wetu kama wizara kwa
kushirikia na wadauwengine wenye nia njema kama wizara kwa kushirikiana na
wadau wengine wenye nia njema kama Samsung ambao watatusaidia kugundua njia za
kutokomeza vitendo hivi vibaya,” alisema na kuongeza;
“Vifaa vinavyoingia sokoni kinyume
cha sheria siyo tu zinazorotesha uchumi bali pia zinawadhulumu Watanzania haki
yao kama wateja walengwa.”
Profesa Mbarawa alisema wao kama
Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wanatambua mchango wa Samsung
Electronics Tanzania katika kuleta mabadiliko ya kiteknolojia kupitia bidhaa
zake mbalimbali.
No comments:
Post a Comment