Kagera
Walimu wawili wanaojitolea Shule ya
Msingi Msali, Kata ya Nyakahura, Wilayani Biharamulo, mkoani Kagera wanatumia
vipande vya mihogo mikavu na mkaa kuandikia ubaoni baada ya kukosa chaki.
Wakizungumza shuleni hapo, walimu hao
walisema hawana chaki za kuandikia na kwamba wanatumia vitabu viwili vya hesabu
na Kiswahili kufundishia wanafunzi 200.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Evelina
Jeremiah alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka jana kutokana na uwapo wa watoto
wengi ambao hawajaenda shule, lakini haijasajiliwa.
“Shule haijasajiliwa, lakini
inaendelea kutoa elimu kwa watoto katika mazingira magumu,” alisema Mwl.
Jeremiah.
Alisema wazazi walianzisha banda la
kuwafundishia watoto kusoma, kuandika na kuhesabu hali iliyosababisha kuajiri
vijana waliomaliza kidato cha nne.
No comments:
Post a Comment