Na Mwandishi wetu
Watoto wawili wemejeruhiwa mmoja kwa
kuvunjika mkono baada ya kuangukiwa na ukuta kufuatia mvua kubwa iliyoambatana
na upepo mkali kunyesha katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Diwani wa Kata Guta wilayani Bunda,
Mwita Mang’era, alisema mvua hiyo ilinyesha katika kijiji cha Nyabehu na
kusababisha madhara kwa watoto hao wawili.
Mang’era alifafanua kuwa mvua hiyo
ilinyesha juzi kwa takriban saa tatu mfululizo.
Aliwataja watoto waliojeruhiwa ambao
ni familia moja kuwa ni Wambura Wambura(9) na Maswi Wambura(4), aliyevunjika
mkono.
“Watoto hao walikuwa ndani ya nyumba
wakati mvua hiyo ikinyesha,” alisema.
Kwa mujibu wa Mang’era, mbali ya
watoto hao kujeruhiwa , pia mvua hiyo ilibomoa nyumba 23 kijijini hapo na
kusababisha wanafamilia zaidi ya 140 kukosa mahali pa kuishi pamoja na kubomoa
ofisi ya kijiji.
No comments:
Post a Comment