Na mwandishi wetu
Walimu wawili wa Shule ya Sekondari
ya Embarway wanashikiliwa na polisi wilayani Ngorongoro wakituhumiwa kufanya
mtihani wa kidato cha nne ofisini.
Licha ya walimu hao kukamatwa pia
walikuwa wasimamizi wa ndani kwenye shule hiyo, wameondolewa kutokana na
uzembe.
Kaimu ofisa elimu wa Wilaya ya
Ngorongoro, Chacha Megewa alidai walimu hao, Jackob Jadie na Reginald Boniface,
walikamatwa wakati wakifanya mtihani wa historia.
Alisema walikamatwa Novemba 5 na
msimazi mkuu wa mitihani, Faustine Bura baada ya kuingia ghafla katika ofisi ya
mwalimu mkuu.
“Msimamizi alikuwa anafuata moja ya
fomu ofisi ya mkuu wa shule, baadaye aliita polisi na kuwakamata,” alisema.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas jana hakupatikana kuelezea tukio hili, lakini polisi Kituo
kidogo cha Ngorongoro ilithibitisha kukamatwa kwa walimu hao.
No comments:
Post a Comment