Benki ya NMB imefadhili jukwwaa la uwekezaji
katika Ziwa Tanganyika linalo lenga kuwahamasisha wafanyabiashara wakubwa
kuwekeza katika ukanda huo ili kuinua nuchumi wa watu wa ukanda huo
Katika uzinduzi wa juma hilo uliofanyika
mwishoni mwa juma na kuwakusanya wafanyabiashara kutoka Kampuni 23 za uwekezaji
za mataifa 30 duniani, NMB pia ilitangaza nia ya kushirikiana na serikali
kupambana na umasikini.
Kuhusu ufadhili wa jukwaa hilo benki hiyo imesema
imelenga kushiriki jitihada za wakazi wa mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma
inayozunguka ziwa Tanganyika katika vita dhidi ya umasikini.
“Kwetu sisi NMB hurudisha kidogo kwa jamii
faida tunayoipata katika biashara ni
faraja yetu. Tumekubaliana na serikali
kwamba popote itakapoanzisha wilaya au mkoa mpya, tutachangia maendeleo ya
uchumi wa eneo husika kwenye nyanja za elimu na afya.”
No comments:
Post a Comment