Kilimanjaro
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro
limemtia mbaroni mganga mmoja wa jadi anayedaiwa kuteka watoto kwa njia za
kishirikina kwa ajili ya kutolewa kafara.
Mbali na mganga huyo, pia wametia
mbaroni mwanamke mmoja, anayedaiwa kusuka mipango ya kutekwa nyara kwa watoto
na kuwahifadhi kwa mganga huyo.
Mganga huyo ambaye anayedaiwa ni
mwenyeji wa mkoani Mbeya, alikutwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13,
akiwa tayari amepumbazwa tayari kumpeleka Mbozi mkoani Mbeya.
Mtoto huyo aliyemaliza darasa la saba
mapema mwaka huu Shule ya Msingi Majengo katika Manispaa ya Moshi ni miongoni
mwa waliofaulu katika mtihani wa Taifa.
Kwa mujibu wa habari hizo, mganga
huyo anadaiwa kushirikiana na mwanamke mmoja, mkazi wa TPC kula njama za
kumteka mtoto huyo.
“Huyo mwanamke ndiye alishirikiana na
huyo mganga kumteka mtoto kwa lengo la kumpeleka Mbozi, mkoani Mbeya na ajabu
ni kwamba naye alikuwa akishiriki kumtafuta,” imedokezwa.
No comments:
Post a Comment