Na Mwandishi wetu
Watanzania wametakiwa kuachwa huru
kutoa maoni ya Katiba inayopendekezwa na chama au asasi yeyote ili kujenga
taifa imara.
Aidha, serikali imetakiwa
isiharakishe kura ya maoni ili kutoa fursa ya kufanyika kwa maandalizi ya
kutosha ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa
Asasi ya Afrikan Community Development Network (Afrocod), Vicent Mughwai,
alisema viongozi na wanasiasa hawapaswi kuwashinikiza wananchi watoe maoni ya
mapendekezo wanayoyataka wao kwa maslahi yao badala yake wawaache wachangie
kile wanachokiamini.
No comments:
Post a Comment