Tuesday, November 18, 2014

Airtel yaendelea kusaidia sekta ya elimu

Simiyu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imesaidia jitihada za serikali kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi katika shule ya sekondari Baariadi iliyoko mkoani Simiyu.

Msaada huo wenye thamani ya Sh. Milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanao soma masomo hayo shuleni hapo.

Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Bariadi, Erasto Sima alisema shule nyingi wilayani hapa zimekuwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masosmo ya sayansi, licha ya kwamba pia kuna uhaba wa walimu wa masomo hayo.

 “Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya sayansi wilayani Bariadi hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu wa sayansi.

 “Uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa Bariadi “ alisema Sima.


Aidha Sima ameishukuru Airtel kwa kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo ufaulu wake umekuwa mdogo, hali inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.

No comments: