Friday, November 21, 2014

Serikali yapiga mnada madini

Arusha
Serikali imeuza kwa mnada aina mbalimbali ya madini yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 milioni yaliyokamatwa wakati yakitoroshwa nje ya nchi.

Mnada huo uliendeshwa jana na mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa madini, Richard Kasesela akisaidiana na maofisa wa Wakala wa Ukaguzi na Madini (TMAA), wakati wa maonyesho ya kimataifa ya madini yanayoendelea jijini Arusha.

Meneja uthamini wa madini kutoka TMAA, George Kaseza alisema madini yaliyopigwa mnada yalikamatwa kwenye vituo mbalimbali vya ukaguzi, vikiwemo viwanja vya ndege na maeneo ya mipakani.

“Madini haya yalikamatwa yakisafirishwa bila vibali maalumu vinavyoruhusu yakauzwe nje ya nchi wala kulipwa ushuru na kodi ya Serikali,” alisema Kasesela.


Alisema Serikali imefikia hatua ya kupiga mnada madini hayo baada ya kuyataifisha kutokana na amri ya mahakama baada ya watuhumiwa waliokamatwa wakisafirisha nje ya nchi kutiwa hatiani na baadhi kuhukumiwa vifungo au faini.

No comments: