Mwanza
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Mkoa wa Mwanza imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara
watakaokaidi agizo la serikali la kutumia mashine za kielektroniki (EFD) kutoa
risiti za uuzaji wa bidhaa.
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza,
Peter Shewiyo, alisema hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya "Mlipa kodi" Kanda ya
Ziwa, yaliyofanyika jijini hapa juzi.
Shewiyo alisema hawatasita
kuwachukulia hatua wafanyabiashara waatkaoshindwa kufuata kanuni na sheria
ambazo zinaelekeza kutumia mashine hizo, kwa kuwa kufanya hivyo kunaikosesha
serikali mapato.
Alisema wafanyabiashara wakitumia
mashine hizo zitawapunguzia wizi, hivyo kuongeza pato la taifa na kuwanufaisha
wao katika kutunza takwimu kwa usahihi.
“Mfanyabiashara yeyote ambaye
hatumii mashine za EFD kisheria
hairuhusiwi kufanya biashara na endapo tukikuta mfanyabiashara ambaye biashara
yake ni kuanzia Sh. Milioni 18 tutamshtaki,” alisema.
No comments:
Post a Comment