Arusha
Serikali imesema itaratibu
uanzishwaji wa chama cha wafugaji nyuki nchini, ambapo kwa kuanzia imeteua
kikosi kazi kwa ajili ya shughuli hiyo.
Hayo yameelezwa juzi na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakati akifungua kongamano la nyuki na
ufugaji nyuki, (APIMONDIA), ambapo alimteua Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko
Kone kuwa mwenyekiti wa kikosi kazi cha uanzishwaji wa chama hicho.
“Wakati akifungua kongamano hilo
ambalo ndilo la kwanza kabisa kufanyika barani Afrika, Waziri Mkuu aliagiza
kuanzishwe chama cha wafugaji nyuki hapa nchini hivyo kwa mamlaka
niliyokabidhiwa natangaza rasmi kuwa serikali ndiyo itaratibu uanzishwaji wa
chama hicho,” alisema.
Mbali na Kone, Nyalandu pia alimteua
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Juma Mgoo kuwa
katibu wa kikosi kazi hicho.
Aliwataja wajumbe wa kikosi kazi
hicho kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa TFS, Esther Mkwizu, mjumbe kutoka uongozi
taasisi isiyo ya kiserekali ya wafugaji nyuki na mwakilishi wa wasomi ambaye
alisema atawakilisha mawazo ya wasomi katika uaznishwaji wa chama hicho na
uendelezaji wa sekta ya nyuki kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment