Mkurugenzi Mkuu wa Serengeti Breweries
Ltd, Steve Gannon, (kulia), Mwenyekiti wa mtaa wa Mkamba, Hussein Saleh
Kisalala (katikati) na Mhandisi Damas Premy kutoka Manispaa ya Temeke (kushoto)
wakikata utepe katika uzinduzi rasmi wa kisima cha maji katika zahanati ya
Mkamba wilayani Temeke. Kisima hicho kimefadhiliwa na kiwanda cha bia cha
Serengeti kwa gharama ya shilingi milioni 50.
Na
Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Sekta ya
afya nchini imezidi kupata msukumo baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji
katika zahanati ya Mkamba wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mradi huo
uliozinduliwa jana wilayani humo umefanikiwa baada ya uwekezaji wa Tshs milioni
50 uliofanywa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).
Kutokana na
mradi huo, pia zaidi ya wakazi 80,000 wa Mkamba, sasa watafaidika na maji safi
na salama uliotekelezwa katika mradi wa kampuni hiyo wa “Maji kwa Uhai.”
Mradi huu
unajumuisha kisima cha maji, tenki la maji na pampu inayotumia umeme wa jua na
linauwezo wa kuzalisha hadi lita 4,000 za maji kwa siku.
Mradi huu
mpya pia utasidia katika kuwezesha utoaji huduma endelevu na shughuli nyingine
katika zanahati ya Mkamba ambayo hapo awali lilishindikana kuzinduliwa kutokana
na tatizo la uhaba wa maji masafi na salama.
"Tunafurahia
kuwa kati ya wadau ambao wamechangia kutoa suluhisho la changamoto ya uhaba wa maji,” alisema Bw Steve Gannon,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Serengeti wakati wa uzinduzi.
Kabla ya
mradi huo, upatakinaji wa maji safi na salama katika zahanati hiyo ilikuwa
changamoto, na hali hiyo ilisababisha kuchelewa kwa ufunguzi wa zanahati.
“Tunaungana
na jumuiya hii kusherekea uzinduzi wa mradi huu wa Maji Kwa Uhai hapa Mkamba na
kuleta huduma bora za afya karibu na wananchi,”
aliongezea Gannon.
Bi. Sofia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya
Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kukamilika kwa mradi huo katika kituo
cha afya cha Mkamba ni moja ya hatua muhimu
sana za kuboresha huduma za maji katika hospitali nchini.
No comments:
Post a Comment