Mbeya
Benki ya NMB imetoa msaada wa
madawati 214 wenye thamani ya jumla ya Sh milioni 15 kwa shule za msingi za
Mbata na Azimio na shule ya sekondari Mbeya Day, zote za jijini Mbeya.
Shule ya sekondari Mbeya Day imepewa
madawati 84, shule za msingi Mbata na Azimio zimepewa madawati 65 kila moja.
NMB imekabidhi msaada huo ikiwa ni
sehemu ya mchango wake katika kutatua changamoto ya upungufu wa madawati kwenye
shule mbalimbali.
Akikabidhi msaada huo meneja wa NMB
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Lucresia Makirine alisema benki hiyo inajisikia
fahari kuona inakuwa sehemu ya wadau waliojipanga kusaidia kutatua changamoto
zinazoikabili jamii.
Makirie alisema benki hiyo itaendeela
kushirikiana na jamii ya waakzi wa jiji la Mbeya kwa kusaidia pale inapoweza
ikiwa ni njia ya kurejesha sehemu ya faida kama shukrani kwa jamii ya wateja
wake.
No comments:
Post a Comment