Na Mwandishi wetu
Walinzi wawili wa
usalama wameuawa na mtu aliyekuwa na kisu, nje ya Ikulu ya Rais wa Sudan iliyopo
jijini Khartoum.
Kwa mujibu wa
Msemaji wa Ikulu nchini humo, mvamizi huyo alinyanyua silaha ya mmoja wa walinzi
ndani ya Ikulu hiyo, kabla ya kuonekana
na kuuliwa na mlinzi mwingine.
Alisema mtu huyo
alionekana kuwa na matatizo ya akili. Rais Omar al- Bashar hakuwepo katika aneo
hilo wakati wa uvamizi huo
Bashir aliingia
madarakani mwaka 1989 ambapo mwezi uliopita, alitangaza kuendelea kuwania tena
nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.
Katibu wa Habari na
mawasiliano wa Ikulu, Emad Ahmed alisema mvamizi huyo alipigiwa kelele lakini
hakuacha kushambulia walinzi.
Aliendelea kuwashambulia hadi pale alipopigwa risasi hadi
kufa na mmoja wa walinzi waliokuwepo katika eneo hilo.
Mahakama ya Kimataifa
ya Jinai (ICC) ambayo Sudani haitambui, imemshitaki Rais Bashir, kwa mauaji ya
kimbari yaliyofanyika Darfur, mashtaka ambayo Rais huyo aliyakanusha.
Umoja wa Afrika
(AU) unamuunga mkono Rais huyo katika kukana mashtaka hayo yaliyotolewa na
mahakama hiyo iliyopo The Hague, Uholanzi.
No comments:
Post a Comment