Na Mwandishi wetu
Wanandoa wawili wameuawa kwa
kukatwakatwa mapanga na kutenganishwa vichwa na viwiliwili vyao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera,
Henry Mwaimbambe alisema jana kuwa mauaji hayo yalitokea Novemba 7, mwaka huu
saa 2.30 usiku nyumbani kwa wanandoa hao kata ya Nshamba, wilayani Muleba.
Kamanda Mwaibambe aliwataja marehemu
hao kuwa ni Alhaji Sadick Hamisi(84) na Zamda Sadick(44).
Alisema wakati wanandoa hao walipokuwa
wakijiandaa kupata chakula cha usiku watu wasiojulikana waliwagongea na
kuwataka wafungue mlango.
Kamanda huyo alisema mlango
ulipofunguliwa watu hao waliwashambulia wanandoa hao na kuwaua.
Alisema mtoto mmoja wa marehemu
anashikiliwa na polisi akituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment