Dar es Salaam
Benki ya NMB imezindua tawi jipya katika soko la wafanyabiashara
Tandika Dar es Salaam kwa lengo la kuwasogezea huduma ili waweze kunufaika na
fursa za mikopo kutoka benki hiyo.
Tawi hilo jipya lilizinduliwa jana na Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Sophia Mjema, ambapo kuzinduliwa kwa tawi hilo kumefikisha jumla ya
matawi 160 nchi nzima ambayo yanatoa huduma.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Meneja wa NMB kanda ya
Dar es Salaam Salie Mlay, alisema katika wilaya hiyo kuna idadi kubwa ya
wafanyabiashara ambao walikuwa wanashindwa kuhifadhi fedha zao kwa urahisi ndio
maana benki hiyo ikalazimika kusogeza huduma.
“NMB imezindua tawi
Tandika sokoni kwa ajili ya wafanyabiashara na wananchi wa eneo hilo ambapo
litakuwa linatoa huduma zake hadi saa 12 jioni na siku za mapumziko pia
litakuwa linatoa huduma kama kawaida,”alisema Mlay.
Alisema benki hiyo mpaka sasa ina matawi yake 160 kwa nchi
nzima na ATM 500 kwa lengo la kufikisha huduma kwa wananchi wao kwa lengo kuu
kila mwnanchi aweze kufika benki kuhifadhi fedha zake sio kuweka chini ya
godoro.
Mlay alisema Dar es Salaam kuna matawi 23 matarajio kuongeza
mengine zaidi kwani wapo mbioni kuzindua matawi mapya kwenye wilaya za Ilala na
Temeke.
No comments:
Post a Comment