Na Mwandishi wetu, Morogoro
Chuo Kikuu Mzumbe leo kinaendesha warsha ya kumuenzi baba wa
Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere.
Warsha hii ni mfululizo wa utaratibu ambao chuo hicho
kimejiwekea ambapo kila mwaka mada mbalimbali huwasilishwa na wasomi na
kujadiliwa ili kuenzi maisha ya baba wa Taifa na kuchangia mawazo ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Chuo Kikuu Mzumbe,
Bi. Rainfrida Ngatunga, mgeni rasmi katika warsha hiyo anatarajiwa kuwa mkuu wa
mkoa wa Morogoro, Dk. Joel Bendera.
Mada kuu ni mtazamo wa Mwalimu kuhusu katiba kama chombo cha
kujenga demokgrasia.
Kongamano hilo linafanyika katika kampasi kuu ya chuo hicho
mjini Morogoro.
“Mada mbalimbali zitajadiliwa msingi ukiwa kutoa mchango kwa
maendeleo ya nchi yetu,” alisema Bi. Ngatunga.
Kwa mujibu wa Mkurungenzi huyo, wadau mbalimbali toka ndani
na nje ya chuo hicho wanatarajiwa kuhudhuria warsha hiyo.
Mada zitawasilishwa na wanazuoni wa Mzumbe na toka nje ya
chuo hicho.
No comments:
Post a Comment