Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
Tanzania imepewa changamoto kufikiria namna ya kuandaa kada
ya viongozi watakaokuwa na uwezo wa kuongoza kutokana na changamoto na mahitaji
ya karne ya 21.
Mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya uongozi, Bw. John Knights
amewaambia waandishi wa habari jana kuwa huu ni wakati muhimu sana kwa Tanzania
kutafakari, kama taifa, jinsi ya kuwa viongozi wa kisasa kwa ajili ya kizazi
kijacho.
Mtaalamu huyo alikuwa akiongea wakati wa semina ya maswala ya
uongozi mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
Semina hiyo ya siku mbili iliyoanza jana imeandaliwa na
Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) na inalenga kuwawezesha washiriki ambao
ni viongozi katika taasisi mbalimbali mbinu mpya za uongozi.
Mtaalamu huyo alisema ni lazima viongozi wawe tayari
kubadilika kwanza wao kutoka ndani ya mioyo yao badala ya kila mara kuwaambia
watu nini cha kufanya.
Hivyo ndivyo mtu anaweza kuwa kiongozi bora,” alisema.
Mtaalamu hyo ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi ya Leadershape
ya nchini Marekani alisema katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, dunia
imebadilika kwa kiwango kikubwa hasa kutokana na matumizi ya mtandao wa
intaneti na kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa kila mmoja.
Alisema, zamani kiongozi alichukuliwa kujua kila kitu na
kuwaambia watu cha kufanya, hali ambayo amesema imebadilika kwa sasa.
No comments:
Post a Comment