Dar es Salaam
Wakati wafanyabiashara wakiendelea
kumiminika eneo hatarishi la mitambo ya umeme ya Ubungo, uongozi wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), ukidai Halmashauri ya Kinondoni, Songas, Sumatra na
Polisi ndio inahusika na usalama wa eneo hilo.
Eneo la Ubungo kwenye mitambo ya gesi
ya Songas ni kati ya maeneo hatarishi ambayo hayapaswi kuwa na mkusanyiko
mkubwa wa watu hasa nyakati za jioni na usiku kama ilivyo sasa.
Wakati hali ikiwa mbaya katika eneo
hilo, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na Kikosi
cha Usalama Barabarani wamedai kuwajibika kuwabana machinga, bodaboda na
madereva wa mabasi ya usafiri watakaosimama katika maeneo hayo yenye msongo
mkuu wa umeme.
Msemaji wa shirika hilo, Adrian
Severin kwa upande wake amesema eneo linalohusu Tanesco, wamefanikiwa
kuzungushia uzio.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda alisema kwa sasa wanaandaa mpango wa kuwazungushia uzio eneo hilo au
kuweka utaratibu ambao utawafanya wasionekane eneo hilo kwani ni kati ya maeneo
hatari huku SUMATRA wakiahidi kuendeleza “operesheni kamatakamata.”
No comments:
Post a Comment