Gairo
Wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) ina mpango
wa kununua tani 2,500 za mahindi katika
Wilaya ya Gairo.
Akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani
jana, Kaimu Ofisa kilimo wa Wilaya, Milaho Cuthbert alisema NFRA itanunua
mahindi kwa Sh500 kwa kilo.
Cuthbert, alisema ununuzi huo utafanyika katika kata 10 na
mgawanyo wa tani zitakazonunuliwa kwa kila kata utazingatia wastani wa mavuno
ya mahindi kwa kila Kata.
Akizungumzia mpango wa ruzuku ya pembejeo za kilimo, Cuthbert
alisema katika utekelezaji wa mpango huo kwa msimu wa 2014/2015, Serikali
imeweka utaratibu wa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wakulima wa mikoa 24 kwa
ajili ya mazao ya mahindi na mpunga.
Alisema mikopo hiyo itatolewa kupitia benki za biashara za
wananchi ambazo zitasaini mikataba na vikundi vya wakulima hao.
Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya wakulima wameishukuru
serikali kwa kuwahakikishia ununuzi wa mahindi yao na kwa kuwapatia soko la
uhakika.
No comments:
Post a Comment