Mtwara
Kampuni tanzu ya taasisi ya Aga Khan
Foundation (AFK), Benki ya Diamond Trust Tanzania Limited (DTBT), imezindua
tawi jipya katika Manispaa ya Mtwara kwa lengo la kukuza uchumi kwa mikoa ya
kusini mwa nchi.
Akizindua tawi hilo mkoani hapa jana,
mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DTBT, Abdul Samji alisema Aga Khan
Foundation imejizatiti kuunga mkono juhudi za wakulima wadogo na wajasiriamali
katika mikoa hiyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo,
kufunguliwa kwa tawi hilo kunaleta changamoto kwa programu ya maendeleo ya
Taasisi ya Aga Khan ambayo imedhamiria kuboresha maisha ya wananchi wengi wa
vijijini katika eneo hilo.
“Kufunguliwa kwa Tawi la DTB Mtwara
ni utekelezaji wa hamu na shauku yetu kuwa sehemu ya ukuzaji uchumi kwa mikoa
ya kusini.”
Alisema DTB inakuwa benki ya nane ya
kibiashara kufungua tawi kwenye Manispaa ya Mtwara ikitoa huduma kikamilifu,
wakati huohuo ikiwa na mikakati ya kuelekeza nguvu zake kwa wafanyabiashara
ndogondogo na wajasiriamali.
No comments:
Post a Comment