Mbeya
Maofisa mazingira katika wilaya za mikoa ya
Iringa na Mbeya wametakiwa kuacha kuwabembeleza wawekezaji wasiozingatia sheria
za uhifadhi wa mazingira.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala
wa Mkoa wa Mbeya, Costantine Mushi, wakati akifungua mafunzo ya siku tano
yaliyoshirikisha maofisa mazingira kutoka wilaya 14 za mikoa hiyo, Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Mushi alisema wapo baadhi ya wawekezaji wa
sekta za madini na n ishati wasiozingatia sharia ya mazingira ya mwaka 2004
inayotaka shughuli yoyote ya maendeleo kuendana na uhifadhi wa mazingira na
hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
Alisema kuwa maofisa wa mazingira wanatakiwa
kusimamia sheria za mazingira kwa kuhakikisha kuwa zinafuatwa ikiwa ni pamoja
na kuwachukulia hatua kali wawekezaji wasio fuata sheria hizo.
Alisema, katika sekta ya nishati, kuna
shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi unaoendelea sehemu mbalimbali nchini
katika nchi kavu, kwenye ukanda wa bahari, katika maji ya kina kirefu baharini
(deep sea), na kwenye maziwa na kusisitiza kuwa, hii ni changamoto kwa maofisa
mazingira katika kutoa ushauri na kuhakikisha kuwa binadamu na viumbe hai
hawaathiriki na uwekezaji huo.
No comments:
Post a Comment