China na Marekani zimeweka wazi mipango yao mipya ya
kupunguza hewa chafu, wakati viongozi wa nchi hizo walipokutana mjini Beijing.
Rais
wa Marekani,Barack Obama ameweka malengo ya kupunguza kiasi cha gesi hiyo kwa
26%-28% ifikapo mwaka 2025,tofauti na kiasi kilichowekwa mwaka 2005.
China haikuweka
lengo maalum isipokua amesema ina nia ya kupunguza kiwango cha gesi hiyo
ifikiapo mwaka 2030.
Hii ni mara ya
kwanza kwa China, ambayo ni nchi inyoongoza kwa uchafuzi wa hali ya hewa kuweka
muda maalum wa kupunguza hewa ya ukaa.
Taarifa hii imekuja
wakati huu ambapo Obama amefanya ziara ya kiserikali mjini Beijing, baada ya
mkutano wa bara Asia.
Tangazo hili ambalo
halikutegemewa kutoka kwa nchi hizo mbili ambazo hutoa 45% ya hewa chafu
litachochea mwamko wa makubaliano ya kupunguza hewa chafu baada ya mwaka 2020,
maridhiano yanayotarajiwa kutamatishwa mjini Paris mwakani.
No comments:
Post a Comment