Pwani
Wanafunzi 70 wa shule ya Msingi
Filbert Bayi iliyopo mjini Kibaha, mkoa wa Pwani, wamenusurika kuteketea kwa
moto baada ya mabweni mawili ya shule hiyo kushika moto na kuungua kabisa.
Moto huo unaodhaniwa ulitokana na
hitilafu ya umeme, ulizuka ghafla shuleni hapo kuanzia katika bweni namba nne
la wasichana, ambalo ni moja ya mabweni ya wanafuzni hao kuanzia saa 8 za usiku
wa kuamkia jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo,
Filbert Bayi alisema ni mapema kueleza thamani halisi ya madhara
yaliyopatikana, lakini kikubwa alishukuru wanafunzi wote wapo salama hakuna
aliyejeruhiwa na moto huo.
“Moto umeshatokea, namshukuru Mungu
wanafunzi wangu wapo saalma, sijapata madhara kwa watoto na naomba mnipe muda
wataalamu wafanya uchunguzi kwanza, ikiwamo na mimi kufanya tathmini ya hasara
iliyopatikana kisha nitazungumza...Nitawaeleza kila kitu,” alisema Bayi.
No comments:
Post a Comment