Dodoma
Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya
Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi unaweza kuwa na manufaa kwa Watanzania
iwapo sekta binafsi itapewa kipaumbele katika kusimamia na kuendesha miradi
mikubwa ya uchumi.
Muswada huo uliwasilishwa jana na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu
wakati wa maoni ya wapinzani yaliowasilishwa na Mbunge wa Viti maalumu
(CHADEMA) Pauline Geku.
Akichangia muswada huo baada ya
kuwasilishwa bungeni mjini Dodoma jana, mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia
alisema wakati Serikali ikiwasilisha muswada huo, inatakiwa kukubaliana na
ukweli kuwa inahitaji kujihakikisha kwanza; inaaminika na pili inakuwa na
uhakika wa ufanisi katika utekelezaji wake.
Alisema sifa hizo mbili muhimu ndizo
zinazoipa naafsi ya kuaminika kwa kujihakikishia usimamizi na utekelezaji wa
sifa zote za mikataba ya ushirikiano na sekta biinafsi, hivyo kuvutiwa zaidi
sekta binafsi kuingia katika ujenzi wa uchumi.
Alieleza tatizo kubwa ni kutokuwa na
vipaumbele sahihi na kutoa mfano wa Bandari ya Dar es Salaam aliyoilezea kama
itaendeshwa vizuri chini ya mwekezaji makini, inaweza kuhudumia bajeti yote ya
serikali.
No comments:
Post a Comment