Dar es Salaam
Shirika la Posta Tanzania (TPC),
limeweka saini makubaliano ya ushirikiano katika utoaji huduma kwa umma na
Kampuni ya simu ya Zantel.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya
kukamilika kwa utafiti wa majaribio wa utendaji uliofanywa Zanzibar na mkoani
Dodoma.
Akizungumza katika hafla fupi ya
makubaliano hayo, yaliyofanyika jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TPC,
Deos Mndeme, alisema makubaliano hayo yanatokana na malengo ya shirika hilo,
kuwafikia wananchi wengi kwa kiwango bora cha huduma na kwamba ni muhimu
kushirikiana na kampuni nyingine ili kuboresha huduma hizo.
Mndeme alisema wamehamia kwenye
utoaji huduma inayohusisha Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), huduma
ambayo itarahisisha utendaji kazi wa shirika na kuongeza faida maradufu
kutokana na uharaka wake.
Alisema waliamua kuchagua Zantel
kufanya nao kazi, hasa kwenye masuala yanayohusu huduma za mtandao kutokana na
ubora wake katika teknolojia hiyo.
No comments:
Post a Comment