Monday, November 10, 2014

Wakulima wengi watumia zana duni



Na Mwandishi wetu

Licha ya mkoa wa Katavi kujijengea heshima ya kuwa miongoni  mwa  mikoa inayozalisha chakula kwa wingi, bado asilimia 80% ya Wakulima mkoani humo wanatumia zana duni za Jembe la mkono.

Katavi ni maarufu kwa kilimo cha mazao ya chakula ya mahindi, mpunga, muhogo, ndizi, maharage na viazi na mazao ya biashara ni kahawa, tumbaku, alizeti, ufuta na michikichi.

Haya yalibainishwa na Katibu Tawala Msaidizi Sekretarieti ya Mkoa (Uchumi), Shenal Nyoni katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi yaliyo fanyika hivi karibuni.

Alibainisha kuwa bado matumizi ya zana bora za kilimo mkoani humo yako nyuma.

Aliongeza kuwa matumizi ya wanyama kazi mkoani humo ni asilimia 15% tuna Matrekta makubwa na madogo ni asilimia 15% tu.

Aliongeza kuwa Idara ya Kilimo imeweza kuhakikisha kuwa vijiji vyote 124, vina daftari la mkulima na kuwa mfano wa kuigwa nchini.

Katika msimu huu wa kilimo, wakulima wamevuna tani 510,248 za mazao mbalimbali ya chakula Mahitaji halisi ya chakula kwa wakazi wote wapatao 634,773 ni tani 190,430, hivyo kuwa na zaidi ya tani 319,818 za mazao mbalimbali, ambapo ziada ya mahindi pekee na tani 289,413.

No comments: