Dar es Salaam
Ukosefu wa mbinu za kuboresha bidhaa,
mtaji mdogo, matatizo ya afya na ukosefu wa mbinu za kuendeleza mikopo midogo
ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake waliojiajiri katika shughuli
za usindikaji vyakula na utengenezaji wa bidhaa za mikono.
Hayo yalibainishwa na wanawake
wajasiriamali kutoka kikundi cha Vimosewa nchini India ambao wako nchini kwa
warsha ya siku mbili kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wanawake
wajasiriamali wa Dar es Salaam.
Akizungumzia uzoefu katika sekta ya
ujasiriamali kutoka India, Mirai Chatterjee alisema wanawake wengi waliojiajiri
wanashindwa kuendelea kutokana na kukosa ujuzi wa namna ya kuongeza thamani kwa
bidhaa wanazozalisha ili kuvutia soko kubwa zaidi.
Alisema changamoto ya mitaji pia
huwakabili wajasiriamali wengi, hivyo kuwataka wale wa nchini kuanzisha vyama
vyao vya kuweka na kukopa, jambo litakalowawezesha kujiongezea mtaji kwa kulipa
riba nafuu.
“Tumenza harakati hizi za kujikomboa
kiuchumi, takribani miaka 30 iliyopita. Pamoja na ukongwe tuliokuwa nao, bado
tuna changamoto ndogondogo zinatukabili, alisema.
No comments:
Post a Comment