Na mwandishi wetu
Watu watano wa kijiji cha Matui, Kata
ya Matui Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wamepoteza maisha na mwingine
kujeruhiwa kutokana kuibuka mgogoro kati ya wakulima na wafugaji uliodumu kwa
muda mrefu.
Chanzo cha mauaji hayo kimeelezwa
kuwa ni mkulima mmoja, Hassani Nkondeja (52) kuuawa na watu wanaodaiwa kuwa ni
wafugaji (Wamasai) akiwa shambani kwake kisha mwili wake kutupwa kwenye shimo
kutoka eneo alilouawa.
Wengine waliouawa ni pamoja na Julias
Ibuma(54) na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Jobu ambaye amedaiwa
kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni huku mwingine mwanamke ambaye jina
lake halikufahamika mapema.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Manyara, jitihada za kuzuia mapigano hayo zinaendelea na kwamba kundi kubwa la
wananchi linakimbilia polisi na maeneo ya nyumba za ibada kunusuru maisha yao.
No comments:
Post a Comment