Dar es Salaam
Benki ya EXIM Tanzania, imeendelea kutanua
wigo kwa wateja wake nchini kwa kufungua tawi jipya mtaa wa Lumumba, jijini Dar
es slaam.
Tawi hilo la Ushirika linaongeza idadi ya
mtandao wa matawi ya Benki hiyo ambayo yameendelea kusambaa nchi nzima.
Akizungumza wakati wa hafla fupi jijini Dar
es slaam jana,
Mkuu wa kitengo cha uperesheni wa Exim, Eugen
Masawe, alisema tawi hilo jipya linaipa
fursa nyingine Benki kutoa huduma zake za kipekee kwa wateja wake.
“Tunayo furaha ya kutangaza kuwa tawi la Ushirika
sasa limefunguliwa rasmi.kutokana na urahisi wa upatikanaji wa huduma “ alisema
Masawe.
Alisema tawi hilo jipya ni uthibitisho pekee
wa ukuaji thabiti wa biashara ya Benki yake, ongezeko la idadi ya wateja na jitihada
zake za kutoa huduma za kipekee kwa wateja wake na jamii yote ya biashara nchi
nzima.
Tumekuwa na mkakati wa kumuweka mteja mbele,
ambavyo umetuwezesha kupeleka huduma zetu pale ambapo pana wingi wa wateja
wetu.
No comments:
Post a Comment