Shinyanga
Wafanyabiashara Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametaka
serikali ikae pamoja na Taasisi binafsi za fedha ya ikiwemo mabenki
yanayojishughulisha na kutoa mikopo kwa wajasiriamali kuweza kujadili masuala
ya riba zinazotozwa kutokana na kuwa kikwazo cha kukuza mitaji yao wanapokopa.
Ombi hili limetolewa hivi karibuni katika risala yao katika
ufunguzi wa Hotel ya Submarine iliyopo mjini Kahama na kuiomba serikali
kuangalia riba zinazo tozwa na masharti ya mikopo kwa wajasiliamari kwa kuwa
yamekuwa kikwazo cha wananchi kutumia fursa hiyo.
Akisoma risala hiyo Mkurugenzi wa Hoteli hiyo ya Submarine
yenye hazi ya nyota tatu, Bw Nyorobi Gisabu, alisema pamoja na sera nzuri za
CCM, serikali kwa upande wake inawajibu wa kuwajali wajasiriamali kwa kukaa
pamoja na taasisi za fedha na kuangalia taratibu zao za mikopo ziweze
kuwasaidia kukuza mitaji na kuchangia pato la taifa.
Bwana Gisabu alisema changamoto inayowakabili wajasiriamali
wengi katika taasisi za fedha ni juu ya masharti ya mikopo na riba zinazo tozwa
wanapokuwa wamekopa na kuiomba serikali kukaa pamoja na kuweza kuangalia mambo
hayo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw
Ally Rufunga, alisema ni kweli masharti
wanayopewa wajasiriamali na taasisi za mikopo na riba zinazotozwa bado
yameendelea kuwa tatizo kwao na kuahidi kuyafikisha serikalini ili iweze kuona
namna ya kuyatatua.
No comments:
Post a Comment