Monday, November 10, 2014

Mahakama ya Mwanzo yataketezwa



Na Mwandishi wetu

Mahakama ya Mwanzo ya Riagoro wilayani Rorya mkoani Mara imechomwa moto na watu wasiojulikana  na mali na nyaraka mbalimbali zimeteketea.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya, Lazaro Mambosasa alisema tukio hilo ni la usiku wa kuamkia Novemba 8.

Uchunguzi unaonyesha mahakama hiyo haina umeme na inasadikiwa imechomwa na wahalifu wanaotuhumiwa katika mahakama hiyo.

Moto huo uliteketeza  samani na vielelezo katika ofisi ya makarani. Hata hivyo, kwa upande wa ofisi ya Hakimu, mafaili yalinusurika kuteketea baada ya wananchi kufika na kuzima moto huo wakisaidiana na Polisi wa Kituo cha Utegi.

“Tumepeleka askari wetu wa uchunguzi katika maeneo hayo ili kuweza kupata wahusika ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.” alisema Mambosasa.

No comments: