Dodoma
Fedha taslimu Sh milioni 41.704 zilipatikana katika mwaka
2001-2014 kutokana na gawio la asilimia 20 inayopatikana kutokana na shughuli
za utalii kila mwaka.
Kati ya fedha hizo wananchi wameshachukua Sh milioni 37.117
na Sh milioni 4.587, ambazo ni za mwaka 2012/2013 na 2013/2014, zipo tayari
kugawiwa kwa wananchi muda wowote taratibu za ugawaji zitakapokamilika.
Hayo yalisemwa bungeni mjini hapa jana na Naibu Waziri wa
Maliasili na utalii, Mahamuod Mgimwa alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Muheza
Herbat Mutangi (CCM) aliyetaka kufahamu namna Halimashauri ya wilaya ya Muheza
ilivyonufaika na Hifadhi ya Misitu ya Amani.
Mgimwa alisema kwa mujibu wa sheria inanapotokea mauzo ya
Mazao ya Misitu ya kwenye mpaka wa Hifadhi hiyo, Halimashauri inapewa asilimia
5 ya mapato kutokana na tozo na kwamba Halimashauri ya Wilaya ya Muheza
ilipatiwa sh milioni 18.018 mwaka 2012.
Alisema faida nyingine iliyopatikana ni upatikanaji wa maji
wakati wote, ambapo Halimashauri hiyo inapata mapato kutokana na malipo ya maji
yanayosambazwa kwa watumiaji katika mji wa Muheza.
No comments:
Post a Comment