Kilwa
Wananchi wametakiwa kukataa kutoa
ardhi yao kwa ajili ya kupisha miradi mbalimbali ya wawkezaji kabla hawajalipwa
fidia zao.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana alisema hayo wilayani Kilwa juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Mkapa.
Alisema wapo baadhi ya watu ambao
wamechukuliwa ardhi yao waliyokuwa wanaitumia katika shughuli za uzalishaji
mali ikiwamo kilimo, lakini hadi sasa hawajalipwa fidia.
Kinana aliitaka Serikali kutotumia
nguvu katika kusimamia na kuzuia baadhi ya mambo yanayofanywa kinyume cha
sheria kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment