Dar es Salaam
Tanzania ni nchi ya kwanza kwa Afrika
Mashariki kaika kuvutia uwekezaji kutokana na sera iliyopo ikiwamo kudhibiti
mfumuko wa bei.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na
Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Umoja (UTT), Profesa Joseph
Kuzilwa, wakati akifungua Mkutano mkuu wa tisa wa mwaka wa wawekezaji wa Mfuko
wa Umoja.
Alisema mbali na Tanzania kushika
nafasi ya kwanza, Pia ni ya nane kwa ukanda wa Jangwa la Sahara kwa uwekezaji.
Katika mkutano huo, Profesa Kuzilwa
alisema mfuko huo umekua kwa kiwango cha asilimia 51.2 kutoka Sh 118.3 billioni
mwaka 2012/13 hadi kufikia Sh 178.9 billioni mwaka huu.
“Idadi ya wawekezaji kwenye mfuko huu
imeongezeka na kufikia 117,471 kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, mwaka huu
na kwamba Mfuko wa Umoja pekee umeongezeka kwa kiwango cha asilimia 51.3 kutoka
Sh 162.2 bilioni na wawekezaji kwenye mfuko huo walioongezeka kutoka 106,266
hadi 107,376,” alisema Profesa.
Aliitaja changamoto inayowakabili
kuwa ni mabadiliko ya teknolojia yaliyosababisha meneja wa mfuko kuendelea
kuwekeza katika tehama ili kuendana na ukuzaji wa soko na kufikia matarajio ya
wawekezaji.
No comments:
Post a Comment