Korogwe
Hifadhi ya Mkomazi imemkabidhi Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo mabati 500 yenye thamani ya Sh12 millioni
kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Meenja Ujirani Mwema wa hifadhi hiyo,
Ahmed Mbugi alisema msaada huo ni mwendeelzo wa miradi mingi ya jamii ambayo
wamekuwa wakiitekeleza kwa ushirikiano na wananchi.
Pia, alisema wataendelea kuhamasisha
utunzaji wa maliasili kwa kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi.
Mkuu huyo wa wilaya aliyataka
mashirika mengine ya umma na kampuni binafsi kuiga mfano wa Tanapa kusaidia
maendeleo ya wilaya zenye mbuga.
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen
Ngonyani alisema madiwani wanapaswa kushirikiana ili kuitunza Mbuga ya Mkomazi.
No comments:
Post a Comment