Na Mwandishi wetu, Rungwe
Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi,
Jenister Mhagama amewataka wanafunzi wa shule ya sekondari ya GOD’s Bridge kuongeza
bidii katika masomo kwa kuwa nchi imefika kipindi ambacho hata wachinja kuku wawe na elimu ya kidato cha
nne.
Mh. Mhagama alisema hayo katika mahafali ya
kwanza ya wanafunzi wa kidato cha nne shule hiyo iliyopo wilayani Rungwe, hafla
ambayo aliitumia kufungua shule hiyo. Waziri alisema alishtushwa na tangazo la
kazi za wachinja kuku linalo taja sifa za watu walio faulu kidato cha nne kwa
kuanzia daraja la tatu.
Alisema aliliona tangazo hilo wakati
alipokuwa amepumzika wakati wa safari yake kutoka Dar es slaam kuja Mbeya
. Kwa kweli tangazo lile na dalili
kwamba wakati umefika kwa kila mwanafunzi kukaza buti kwani kila kazi itahitaji
elimu ya kutosha pamoja na ujuzi alisema Waziri Mhagama.
No comments:
Post a Comment