Msajili
Msaidiza wa wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA), Bw. Seka Kasera
(kushoto) akimsikiliza mmoja wa wafanyabiashara wa halmashauri ya wilaya ya
Mbinga mkoani Ruvuma, Bw. Mdaka Mdaka muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi
la usajili wa majina ya biashara kwa wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake
mwishoni mwa wiki. Zoezi hilo limeambatana na utoaji elimu juu ya umuhimu
wa kusajili majina ya biashara na kazi zinazofanywa na wakala huo na limeanza
mkoani Njombe wiki hii.
Na Mwandishi Wetu, Mbinga
Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umesema
mwamko ulioonyeshwa na na wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani
Ruvuma kusajili majina ya biashara zao unatakiwa kuigwa na wengine Tanzania.
“Wakazi wa Mbinga wameitikia vyema tangu siku ya
kwanza tunaingia hapa,”alisema Msajili Msaidizi wa wakala huo, Bw. Seka Kasera
wakati wa wiki ya elimu kwa umma kuhusu kazi za wakala katika mkoa wa Ruvuma
mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Bw. Seka, wengi wa waliojitokeza ni
wajasiriamali wadogo na wakulima wa kahawa ambao kwa kiasi kikubwa wamekua na
mwamko mkubwa wa kusajili biashara zao.
Mbali na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu
kazi za wakala, pia wafanyabiashara katika wilaya husika wanapewa fursa ya
kusajili majina ya biashara zao kwa kutumia mfumo wa kielektroniki uliobuniwa
hivi karibuni.
“Wakulima wamekua na mwamko mkubwa sana katika
zoezi hili na wamekuja kwa wingi sana hapa Mbinga,”aliongeza Kasera.
No comments:
Post a Comment