Mwenyekiti wa Makampuni ya
IPP, Dr. Reginald Mengi (katikati) akiwa na Mratibu wa
Mradi-Surua-Rubella, Lions Clubs Tanzania, Mr. Abdul Majeed Khan (kulia)
na Gavana Mstaafu, Lions Clubs Tanzania, Bw.Wilson Ndesanjo wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella kwa mkoa wa Dar es
Salaam Jumatatu wiki hii.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa
ujumla wamehamasishwa kuzidi kuendelea kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya
surua na rubella ili kujenga taifa lenye watu wenye afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo
dhidi ya Surua na Rubella katika mkoa wa Dar es Salaam Jumatatu wiki hii,
Mwenyekiti wa Baraza la Lions Clubs International, Bw. Abdul Majeed Khan kila
mzazi anatakiwa kuhakikisha mtoto wake anapata chanjo hiyo.
“Tunatambua umuhimu wa chanjo hii kwa watoto...
wananchi waone umuhimu wake,” alisema.
Katika kampeni hiyo, pia zinatolewa dawa za kuzuia
ugonjwa wa matende na minyoo kwa watu wazima.
Alisisitiza kuwa chanjo hiyo inalenga kusaidia kujenga
watoto wenye afya nzuri ili waweze kuja kuwa nguvukazi ya taifa.
Alisema taasisi ya Lions Clubs ni ya kimataifa na
imekuwa ikisaidia maswala mengi nchini na duniani na safari hii kwa Tanzania
imeunga mkono kampeni ya chanjo didhi ya magonjwa hayo ambayo yana kinga.
“Tumekuwa tukisaidia nchini Tanzania watu
kupata huduma ya macho na tayari duniani kote watu wapatao milioni 40
wamesaidiwa,”alisema.
Pia taasisi hiyo hupeleka watoto wenye magonjwa ya
moyo India kupata matibabu na mpaka sasa wamesaidia watoto wa kitanzaia wapatao
300.
No comments:
Post a Comment