Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera, amewaonya
watendaji wanaoshiriki utekalazaji wa Mpango wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf)
awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini kuhakikisha wanachagua walengwa lasivyo
watachukuliwa hatua kali.
Bendera alitoa onyo hilo wakati akizindua
mpango huo katika Manispaa ya Morogogoro na Halimashauri ya Wilaya ya Morogoro
kwa nyakati tofauti mjini hapa.
Alisema mpango huo umekuja kwa ajili ya
kusaidia watu masikini hivyo watendaji wanatakiwa wasirejee makosa yaliyokwishafanywa
na watendaji katika awamu ya kwanza na ya pili kwa maslahi yao kisiasa.
Alisema mpango huo unakusudia kusaidia kaya
masikini baada ya kufanyiwa majaribio katika baadhi ya wilaya nchini
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero
Antony Mtaka alisema endapo watendaji hao watafanikisha watasaidia kurudisha
imani za wananchi kwa viongozi wao.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tasaf, Farij
Mshee alisema mpango huo unatarajia kusaidia watu milioni 6.5 kwa kuwaondolea
umasikini.
No comments:
Post a Comment