Tuesday, October 28, 2014

Mauzo soko la hisa yapungua

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Soko la hisa Dar  es salaam limesema, mauzo ya hisa yamepungua kwa asilimia nane ukilinganisha na mauzo yaliyo fanywa wiki ya juzi .Mauzo hayo yaliyofanywa wiki ya jana ni sawa na shilingi Billion tisa ambapo mauzo hayo ni kuanzia Oktoba 20 hadi 24 mwaka huu .

Akizungumza jana Dar es salaam ofisa habari wa soko hilo, Aleki Ngoshani alisema sababu ya mauzo ya hisa kupungua ni kutokana na idadi ya hisa zilizouzwa zilipungua bei ya kuuzia

Alisema idadi ya hisa hizo ilipungua kwa shilingi milioni 27.62 ukilinganisha na mauzo ya nyuma yaliyopita. Pia alisema kampuni nyingi zimeshuka kwa punguzo la asilimia 1.43.


Sababu nyingine iliyosababisha soko hilo kushuka ni thamani ya hisa nyingi za kampuni kama sigara (TCC), Kampuni ya Swala na Kampuni ya Bia (TBL) kushuka. Maendeleo ya kampuni ya benki imeendelea vizuri kwani benki nyingi zimeongeza  bei ya hisa zao; Benki ya CRDB iliuzwa kwa shIilingi 500, NMB iliuzwa 4720 na Benki ya DCB iliuzwa kwa shilingi 560.

No comments: