Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya simu za
mkononi, Zantel, Bw. Essa Al Haddad (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Bw. Pratap
Ghose (kushoto) na
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Sukhwinder Bajwa (katikati) wakati wa
uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja Zantel lililopo mtaa wa Samora
jijini Dar es Salaam jana.
Na
Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Taarifa
kwamba kuna uwezekano wa kampuni za simu za Vodacom na Millicom International
Cellular inayofanya biashara kama Tigo, kununua asilimia 65 ya hisa za Etisalat
Group katika kampuni ya simu za mkononi ya zantel, zimekanushwa.
Uongozi wa
Zantel umesema taarifa hizo si za kweli.
Jumatano
ya wiki hii, gazeti moja la kiingereza la kila siku liliripoti kuwa kampuni ya
Etisalat kwa kushirikiana na Deutsche Bank AG inaangalia uwezekano wa kuuza
hisa zake asilimia 65, hatua ambayo imezivutia Vodacom Group Ltd na Millicom
International Cellular.
“Hizi ni
taarifa za magazeti tu,” Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel, Bw. Essa Al Haddad
aliwaambia waandishi wa habari jana alipokuwa akifungua duka jipya la Zantel
lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Alifafanua
kuwa badala ya kuuza hisa zake 65, Etisalat Group ilitangaza hivi karibuni
kuongeza hisa zake Zantel kufikia asilimia 85, hilo likiwa ni ongezeko la
asilimia 20.
Asilimia nyingine 15
zinamilikiwa na serikali ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment